Wanamuziki mahiri wa muziki wa Bongo fleva Ali Saleh Kiba pamoja na Nassib Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz wanatarajia kukutana kwenye kamati ya hamasa kwa mchezo wa jumuia ya madola ‘Common wealth Games’ ikiwa ni pamoja na kombe la dunia kwa watu wenye ulemavu ‘Paralympic World Cup’.

Hilo limetokana na uteuzi uliofanywa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa ambaye ameteua takribani watu 13 watakaoitengeneza kamati hiyo.

Kati yao wakiwamo waimbaji hao mahasimu wa muda mrefu kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo fleva.

Michezo hiyo ya jumuiya ya madola kwa mwaka huu, itafanyika huko mjini Birmingham Uingereza, kuanzia Julai 28 hadi Agosti 8 mwaka 2022, mashindano yaliyopewa jina la ‘Barmingham 2022’

Daktari afunguka majeraha ya Feisal Salum
Nandy na Billnass ndoa imeiva