Mfalme Kiba kama anavyoitwa na mashabiki wake amekutana na Ne-Yo nchini Kenya katika jumba linalo-host  ‘Coke Studio Afrika Msimu wa Tatu’.

Kukutana kwa wawili hao kunaashiria mwanzo wa utekelezaji wa collabo kati yao ikiwa ni wiki moja tangu taarifa za kufanya wimbo wa pamoja kutolewa na kuthibitishwa na Ali Kiba.

Kwa mujibu wa Ali Kiba, atarekodi wimbo na Ne-Yo kama sehemu ya mradi huo wa Coke Studio na kutumbuiza kwenye jukwaa moja wakati wa kurekodi msimu huo. Wimbo huo pia utachezwa kwenye vituo vya radio kama wimbo rasmi.

Mbali na Mkali huyo wa Miss Independent, Ali Kiba pia amekutana na wasanii wengine wakubwa wa Afrika ikiwa ni pamoja na Wangechi (Kenya), Dama Do Bling (Mozambique), Ice Prince (Nigeria) na Maurice Kirya (Uganda).

Hii ni mara ya kwanza kwa Ali Kiba kushiriki katika msimu wa Coke Studio Afrika unaowakutanisha wasanii wakubwa wa Afrika  kwa lengo la kurudia nyimbo zao kwa kufanya collabo na kuimba pamoja jukwaani.

CCM Watangaza Kikosi Cha Kumuangamiza Lowassa
Vuguvugu La Usajili Barani Europa