Ali Kiba na Nandy wameng’ara kwenye tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA 2017) zilizofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria.

‘Mfalme Kiba’ ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo mbili nzito kupitia wimbo wake ‘Aje’. Remix ya wimbo huo aliomshirikisha M.I wa Nigeria umempa tuzo katika vipengele vya  Msanii Bora au Kikundi Bora cha RnB na Soul Kiafrika (Best Artist or Group in Africa RnB & Soul) na Wimbo Bora wa Kushirikiana Afrika (Best Africa Collaboration).

Kwa upande wa Nandy ameitoa kimasomaso Tanzania kwa kushinda tuzo hiyo katika kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki.

 

Wasanii wengine wa kike wa Tanzania waliokuwa wanawania kipengele hicho ni Vanessa Mdee na Feza Kessy.

Trump achukia kuitwa 'mzee' na Kim Jong-un
Askari waliobaka watoto wa miezi 18 wakalia kaa la moto