Kama unamshindanisha Ali Kiba na msanii yeyote wa Bongo Flava hapa Tanzania, utakuwa unamkosea kwa kiwango cha daraja la Kwanza.

Mwimbaji huyo ambaye aliweka historia ya kuwa msanii pekee nchini aliyewahi kufanya wimbo na Mfalme wa R&B duniani, R-Kelly amesema kuwa hapaswi kufananishwa na msanii yeyote kwa kuwa hakuna anayemgusa.

Kiba ambaye leo ameachia rasmi wimbo wake mpya wa Lupela, anaamini yuko ngazi nyingine ya kimatafa.

“Usinifananishe na msanii yeyote, hakuna anayenipata , iko hivyo na itabaki kuwa hivyo,” Ali Kiba aliiambia ‘The Sporah Show’.

 

Unataka kumhonga B 12 ili apige wimbo wako redioni? Hiki ndicho atakachokufanyia
G - Nako asakwa na Wasanii wa Kimataifa