Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania, kupitia chama hicho Tundu Lissu, amekitaka chama chake kuendelea kuhubiri demokrasia huku akisisitiza maadili ya chama yazidi kuimarishwa.

Lissu amesema hayo wakati akizungumza katika mkutano alioufanya kwa njia ya mtandao, ambapo amewashukuru wananchi wote waliojitokeza katika kampeni za chama chake na kusema kuwa wananchi ndio waliokuwa nguzo katika kipindi chote cha kampeni.

“Tunachotakiwa kufanya ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa wavumilivu na licha hayo lazima tuhakikishe muungano na ushirika wetu unalindwa ili kufanya hivyo lazima tuhakikishe muungano wa chama na uongozi wake unazingatiwa, lazima tuendelee kukijenga upya na kukiimarisha chama chetu,” amesema Lissu.

Aidha Lissu, amewasisitizia wananchi kutokukata tamaa na kuwapongeza viongozi wa vyama, waliokuwa wagombea mbalimbali katika kampeni  pamoja na timu nzima za kampeni kwa kupambana na changamoto zilizokuwa zikijitokeza na kufanikisha mchakato mzima wa kampeni.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 24, 2020
Jicho la UN laitazama Ethiopia