Edward Lowassa ametoa kauli yake kufutia mauaji ya kikatili ya Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.

Lowassa ameandika hisia zake kupitia mtandao wa Facebook akionesha jinsi alivyosikitishwa na kifo hicho.

“Nimeshtushwa na kusikitishwa na taarifa za msiba wa kijana wetu Alphonce Mawazo, Natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na familia yetu ya UKAWA.Hakika tumeondokewa na mpiganaji,” aliandika Lowassa.

Lowassa atamkumbuka Mawazo kwa jinsi alivyomnadi katika jukwaa la kampeni mkoani Geita, huku akisikika mara kadhaa akimuita ‘mheshiwa rais’ wakati wa kampeni za urais mwezi Oktoba.

Picha: Justin Bieber Amwaga Machozi Jukwaani Kuililia Ufaransa
Dkt. Nchimbi, Ndugai, Mpambano Mkali Uspika