Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakiwa na majeraha ya risasi waliyoyapata kwenye maandamano ya Chadema yaliyotokea Februari  16, 2018.

Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Muliro Jumanne amethibitisha kuwashikilia watuhumiwa hao watatu wenye majeraha ya risasi waliopo katika kituo cha polisi cha Osterbay.

Aidha amesema kuwa watu hao wamejulikana kwa majina kuwa ni Aida Olomi, Isaack Lomanus Ngaja na Erick John wamepelekwa hospitali za Serikali kwa ajili ya matibabu.

Aidha kumetokea na uvumi uliodai kuwa watu hao bado hawajapatiwa matibabu ya majeraha waliyoyapata wakati polisi wakijaribu kutuliza ghasia hizo.

Ambapo dada wa Aida alomi, ameposti kwenye mtandao wake wa Twitter akidai kuwa ndugu yake huyo alipigwa risasi ya mguuni hadi sasa hajapatiwa matibabu yeyote, hivyo ameomba umma kupaza sauti kwani ndugu yake huyo bado yupo Osterbay polisi na kidonda chake kinazidi kuwa kikubwa.

Hivyo Muliro amekanusha taarifa hizo na kusema mpaka sasa hakuna asiyepatiwa matibabu.

 

 

 

Zitto aelezea mazito aliyokutana nayo selo
Mbwa azua taharuki baada ya kugeuka kuwa binadamu