Spika wa Bunge Tukufu la Tanzania, Job Ndugai leo bungeni ametoa neno kufuatia uamuzi uliotolewa leo Septemba 9, 2019 na Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam juu ya kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antipas Lissu.

Ambapo Spika amesema kuwa ni kweli Lissu alikuwa mgonjwa lakini anajitambua, hivyo alikuwa na nafasi ya kutoa taarifa kwa spika juu ya ugonjwa na matibabu yake ambayo ameyafanya kwa kipindi cha mwaka mzima akiwa Ubelgiji.

”Bunge kama hili linaloendelea, wewe uwe unaumwa lakini upo conscious lakini sio mauti uti kiasi hicho, hivi kumjulisha spika tu kuna ubaya gani, Mheshimiwa spika mimi sitaweza kuhudhuria bunge hili la 16 sababu kama unavyojua nipo hospitalini bado naendelea kuumwa, hata ukipiga simu tu si ndio taarifa umetoa, hata ukiandika meseji tu si taarifa umetoa, kwahiyo mengine yote unafanya isipokuwa kumwambia spika, mwaka unapiita nakuona tu…, mengine yote unaweza kufanya lakini kuwasiliana na huyu hufanyi” amehoji Ndugai.

Hata hivyo mahakama imeamua kufutilia mbali kesi ya Lissu na kudai kwamba kesi hiyo ni ya kikatiba hivyo inapaswa kufunguliwa kwa mfumo wa kesi ya uchaguzi na si kwa mfumo ambao alikuwa ameutumia.

Lissu alivuliwa ubunge kwa madai kwamba hakuwa ametoa taarifa rasmi ya alipo, na pia hakuwa amejaza fomu za mali na madeni ya viongozi wa umma.

Mnamo Septemba 7, 2017, majira ya saa 7 mchana Lissu alishambuliwa kwa risasi 38 na watu wasiojulikana ambapo risasi 16 zilimpata katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mguuni, tumboni, na mkononi hali iliyopelekea kufanyiwa upasuaji mara 22 ili kuondoa risasi hizo.

Shambulio hilo lilitokea jijini Dodoma akiwa kwenye gari yake karibu na nyumabni kwake.

Mara baada ya kutokea kwa shambulio hilo Lissu alipelekwa nchini Nairobi kwa matibabu zaidi na baadae kuhamishiwa nchini Ubelgiji ambapo amekaa kwa kipindi chote hiko akiwa anafanyiwa matibabu.

Kufuatia kutokuhudhuria vikao mbalimbali vya bunge kwa kipindi cha mwaka mzima, Lissu alivuliwa ubunge na jimbo lake na kutangazwa kugombewa upya ambapo mrithi wa jimbo la Singida Mashariki kwa sasa ni Miraji Mtaturu ambaye rasmi Mahakama ilimuapisha Septemba 3, mwaka huu na tayari ameanza kutekeleza majukumu yake kama mbunge wa jimbo hilo.

 

 

Mechi ya Simba, Mtibwa yarudishwa nyuma
Taifa Stars isibweteke bado ina kibarua kigumu