Katika hali ya kushangaza, mwanaume mmoja nchini Malawi amegeuka kuwa mfanyabiashara anayefanya kazi ya kuwaondoa usichana (bikira) mabinti na kulipwa fedha na wazazi wao.

Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Erick Aniva, mkazi wa kijiji cha Nsanje nchini humo ameeleza kuwa yeye hulipwa fedha na wazazi wa wasichana hao ili awabikiri kwa maana kuwa ana dawa ya kuwaondoa mikosi kwa njia hiyo.

Kwa mujibu wa Aniva, wanaume wanaofanya kazi hiyo wapo kadhaa katika jamii hiyo na hutambulika kama ‘Fisi’.

Bwana huyo amepata kazi hiyo kutokana na imani iliyopo katika jamii ya kijiji kimoja nchini Zambia ambayo huamini kuwa msichana anapokuwa na bikira baada ya kuvunja ungo ni mkosi. Hivyo, bwana Fisi ndiye anayepewa kazi ya kuwaondoa mkosi kwa njia hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa BBC, Aniva ambaye ni baba wa familia amesema kuwa amekuwa akichemsha mzizi maalum kama dawa (anaouonesha pichani) na baadae kuwabikiri wasichana anaoletewa na kwamba hulipwa kiasi cha dola 7 (sawa na shilingi 153,000 za Tanzania) kwa msichana mmoja.

“Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104. Hii ndiyo tamaduni yetu,” Aniva (Fisi) aliiambia BBC.

Aniva akiwa na familia  yake

Aniva akiwa na familia yake

Alieleza kuwa kwa mujibu wa tamaduni zao msichana anapovunja ungo hufanyiwa sherehe na kufikishwa kwa ‘Fisi’ ili amuondoe ubikira wakiamini anamuondoa mkosi. Katika tukio hilo husindikizwa na watu mbalimbali wa heshima kwake wakiwemo mashangazi wake.

Hii ni ajabu na kweli!

 

Jose Mourinho Akataa Kusaini Jezi Za Chelsea
FC Barcelona Waipokonya Tonge Mdomoni Real Madrid