Msanii wa uchongaji vunyago, Omary Mwariko aliyechonga fimbo aliyokuwa anaishika Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere ameandaa fimbo nyingine kwaajili ya kumkabidhi Rais wa sasa, John Magufuli kama alama ya kumuenzi Nyerere.

Mzee huyo ambaye ni mkazi wa Kilimanjaro amesema, ” Fimbo niliyompa Baba wa taifa ni fimbo yenye uwezo mkubwa wa kusaidia katika mambo mbalimbali ya kitanzania katika mila, jadi na desturi, hii anayokwenda kupewa Magufuli imeongezwa ukali zaidi ili iwaweze mafisadi na wale wanaokuwa hawaeleweki mbele zake.

Akizungumza na Azam tv, amesema ndani ya Tanzania kuna makabila mengi na kila moja lina imani yake. mti unaotumika kutengenezea fimbo hiyo ni mti wa kichifu unao itwa mti wa Mkuru.

Aidha, amebainisha kuwa ana imani kabisa kwa namna atakavyoongea naye Rais ataipokea fimbo hiyo, ila kwanza anataka kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ili amuunganishe aweze kuonana na Rais Magufuli.

 

Chadema yafunguka kususia Uchaguzi Serikali za mitaa
Cristiano Ronaldo atinga anga za magwiji wa soka duniani