Baada ya kutangazwa kwa kifo cha kwanza cha mtanzania kutokana virusi vya covid 19 usiku wa kuamkia leo, familia yake imetoa taarifa kuwa Marehemu Iddi Hashim Mbita atazikwa na Serikali leo mchana.
” Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake, Corona, Serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana” Imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa licha ya familia ya marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kupokea kwa huzuni kubwa na kifo hicho, wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi.
Aidha hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi, kila mtu aomboleze kwake.