Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa si yeye binafsi aliyefungia nyimbo za wasanii kama wengi wanavyochukulia.
Naibu Waziri ameyasema hayo siku mbili baada ya Diamond Platinumz kuukosoa vikali uamuzi ‘wake’ wa kuzifungia nyimbo za wasanii pamoja na msanii Roma Mkatoliki.
Amewataka wananchi na wasanii kuelewa kuwa uamuzi huo ni uamuzi wa mamlaka zinazohusika na sio uamuzi wake binafsi.
“Aliyewafungia wasanii sio Shonza, bali ni mamlaka na kama mlivyoona safari hii hadi Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imengilia kati suala hilo. Sasa mtu anaporusha tuhuma kunilaumu anakuwa hanitendei haki,” Shonza anakaririwa na Mwananchi.
- Ronda Rousey afunguka kuhusu kipigo kilichomtoa UFC
- JPM amtumbua Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi NHC, avunja bodi ya shirika hilo
Shonza aliwataka wasanii wenye malalamiko ikiwa ni pamoja na Diamond, kufuata utaratibu wa kiofisi kuwasilisha malalamiko yao.