Aliyekua waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmet ameachiliwa huru kwa msamaha baada ya kutumikia miezi kadhaa ya kifungo chake.
Olmert ametumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi, pia kujaribu kuzuia mkono wa sheria kufanya kazi yake. Ametenda makosa hayo alipokuwa waziri wa biashara nchini humo.
Olmert alikua waziri mkuu toka mwaka 2006 hadi 2009 na ametajwa kuwa kiongozi wa kwanza aliyeshika cheo cha uwaziri mkuu kufungwa jela huko Israel.
-
Baba yake Michael Jackson apata ajali ya gari, afya yake yaripotiwa
-
Trump awatolea uvivu Korea Kaskazini, ‘imetosha’
Moja ya sababu zilizopelekea kuachiliwa huru ni pamoja na kuwepo kwa wasiwasi kuhusu kudhoofika kwake kiafya.
Aidha, Wizara ya sheria nchini humo ilidokeza kuwa hivi karibuni Polisi walikua wakimchunguza Olmert kuhusiana na tetesi kuwa alifanikiwa kutoa kimagendo nyaraka alizoandika kwa lengo la kuchapisha kitabu.