Aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali Awamu ya Nne, Gregory Teu ambaye pia alikuwa Mbunge wa Mpwapwa Mkoani Dodoma amepoteza ndugu wa familia yake kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Septemba 18,2017, Jijini Kampala nchini Uganda.

Taarifa zinaeleza kuwa, ajali hiyo mbaya iliyosababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine kadhaa imehusisha gari yenye namba T 540 DLC, ambapo tukio hilo limetokea karibu na mto Katonga barabara ya Masaka Jijini humo.

Gari hilo lilikuwa likiwarudisha watu hao ambao ni Watanzania wa familia ya Naibu Waziri huyo aliyewahi kuitumikia Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu ambapo imeelezwa familia hiyo ilikuwa nchini humo kwenye harusi iliyofanyika Septemba 16, mwaka huu jijini Kampala.

“Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19, kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital, Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliopoteza maisha na kunusurika,”umesema ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Tayari Naibu Balozi, Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wa Tanzania wameelekea Nsambya Hospital kuona walio nusurika, hivyo kuahidi kuendelea kutoa taarifa kamili za majeruhi na marehemu hao.

Rooney akumbana na hukumu baada ya kukiri kosa
Watu 7 watiwa mbaroni kwa kupinga mabadiliko ya ukomo wa umri wa rais