Mchekeshaji kutoka nchini Uingereza, Simon Brodkin aliyevamia mkutano wa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter wakati akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa juma hili atafunguliwa mashtaka kufuatia kitendo hicho.

Mamlaka ya jeshi la polisi nchini Uswis, imethibitiha taarifa za kufunguliwa mashtaka kwa mchekeshaji huyo, kwa kosa la kuvamia mkutano wa rais wa FIFA bila kibali maalum hasa ikizingatiwa hakuwa na sifa za uandishi wa habari kama ilivyokuwa kwa wageni waalikwa kutoka katika vyombo vya habari.

Hata hivyo alipopanda jukwaani mchekeshaji huyo alijitambulisha kwa jina Lee Nelson, hatua ambayo bado inaendelea kudhihirisha alikuwa muongo na hakua na dhamira njema katika mkutano huo.

Simon Brodkin, mwenye umri wa miaka 38, amekuwa akifanya matukio mbali mbali ya kuvamia mahala pasipomuhusu, kwani aliwahi kujichanganya na wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wakati wakijiandaa kusafiri kuelekea nchini Brazil kwa ajili ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014. Pia aliwahi kupanda jukwani wakati msanii wa muziki kutoka nchini Marekani Kanye West akitumbuiza jijini London.

AS Roma Yamnyemelea Wojciech Szczesny
UDSM Yamtunukia Rais Kikwete Shahada Ya Heshima Ya Udaktari