Damien Tarel mwenye umri wa miaka 28 amehukumiwa kifungo cha miezi minne gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kufanya ghasia ya makusudi kwa kumpiga kofi rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Awali rais Macron alisema hakuamua kuchukua hatua za kisheria na badala yake aliamua kuliacha suala hilo kushughulikiwa na Chombo husika

Jumanne Juni 8, 2021 Rais Macron alishambuliwa kwa kupigwa kofi na raia huyo alipokuwa ziarani kusini mwa taifa hilo.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, mtu huyo alionekana akimtandika kofi Rais Macron kabla ya kudhibitiwa na maafisa usalama.

Tukio hilo liliibua gumzo kubwa duniani huku wengine wakihoji usalama wa kiongozi huyo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Ngrebada, ajiuzulu
Rais Samia atengua uteuzi wa Chalamila