Mwanamke mmoja mkaazi wa Pennsylvani aliyetajwa kwa jina la Rhonda Shoffner, ametupwa jela leo kwa kosa la kumpiga mwanae wa kike aliyekosea kuelezea mstari wa Biblia, PennLive imeripoti.

Shoffne mwenye umri wa miaka 41 amefungwa jela miaka miwili na nusu baada ya kukutwa na hatia ya kumnyanyasa na kumpiga mwanae huyo mwenye umri wa miaka 13.

Kwa mujibu wa maelezo ya muendesha mashtaka, Shoffne alifanya kosa hilo nyumbani kwake eneo la Middletown na kwamba alikuwa amelewa pombe.

Mtoto wake aliliambia Jeshi la Polisi kuwa mama yake alikuwa amefululiza kunywa pombe kwa siku tatu. Alisema kuwa mama yake huyo alimtisha na kumpiga majira ya saa tisa mchana.

Mtoto huyo alieleza kuwa mama yake alifika nyumbani na kumtaka awapigie simu ndugu zake kadhaa. Lakini kwa bahati mbaya wote hawakupokea simu, ndipo alipochukia na kuanza kumtishia akimlazimisha kupiga magoti karibu na bafu.

“Naomba mama usinipige, sitaki kupiga magoti,” mtoto huyo alilieleza jeshi la polisi, maelezo ambayo yalisomwa mahakamani.

Hata hivyo, aliendelea kumlazimisha kupiga magoti hadi akafanikiwa. Imeelezwa kuwa alimtaka mwanae aeleze Mungu alimwambia nini Ibrahim kuhusu mwanae wa kiume [Isaka]. Mtoto alijibu, “Mungu alimwambia amsamehe mwanae wa kiume.”

“Hapana, Mungu alimwambia Ibrahim amuue mwanae wa kiume,” maelezo ya Polisi yanamnukuu mama huyo na kuongeza kuwa alianza kumpiga kwa kumuinamisha ndani ya bafu akimtaka asahihishe mstari huo.

Essam El Hadary apambanishwa na vijana tuzo ya Afrika 2017
Rais Karia awapa pole Silabu FC