Nyota wa Cosmopolitan, Gilbert Boniface amesema kitendo cha kufungiwa michezo 10 na Bodi ya Ligi (TPLB) kutokana na kilichoelezwa kumshika sehemu za siri mwamuzi kimemvunja sana moyo kwani hakutegemea angekutana na adhabu hiyo.

Gilbert amesema ameshangazwa kwa kiasi kikubwa na uamuzi uliochukuliwa dhidi yake kwa sababu hakufanya kilichoelezwa isipokuwa baada ya KenGold kupata penalti alimwambia tu mwamuzi achezeshe kwa haki mehezo huo.

“Nimetafakari sana kwa nini mwamuzi aliandika katika ripoti yake nimefanya kitendo kama hicho tena angalau angekuwa ni wa kike ila ni wa kiume japo kuwa simkumbuki jina ila anatokea Mwanza, kwangu imeniuma ila sina budi kukubaliana nao.” amesema Staa huyo aliongeza kufungiwa kwake kumemuathiri kisaikolojia kwa kiwango kikubwa kwani michezo 10 ni mingi na mpira ni kazi yake anayoitegemea, hivyo isitoshe pia imemuharibia taswira yake kwa jamii inayomzunguka kutokana na kitendo hicho.

Gilbert pia ametozwa faini ya Sh 500, 000 baada mchezo wa Championship waliopoteza kwa 2-0, dhidi ya KenGold Oktoba 21, uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Idadi ya Watanzania wanaotembelea Hifadhi yaongezeka
Unai Emery aiweka mtegoni Aston Villa