Mwanasiasa wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Nchin Kenya (NASA), Miguna Miguna amefukuzwa nchini humo na kupelekwa nchini Canada kupitia ndege ya KLM, kulingana na wakili wake Nelson Havi na Cliff Ombeta.
Ombeta amesema kuwa aliarifiwa kwamba, Miguna aliingizwa katika ndege iliyokuwa ikielekea Amsterdam na baadaye kuelekea Canada.
“Ni kweli alilazimishwa kuingia katika ndege ya KLM dakika chache tu kabla ya saa nne usiku na tumebaini kwamba anaelekea Canada, huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu,”amesema Dkt. Khaminwa
Aidha, amesema kuwa hajui ni sheria gani iliyotumiwa na serikali kumuondoa nchini humo kwa kuwa katiba inampatia haki kama raia wa Kenya kwa kuwa ni mzaliwa wa taifa hilo,
Hata hivyo, Mkurugenzi wa shirika la ujasusi amesema kuwa, Miguna alikamatwa baada ya kukiri kumpatia kiapo kiongozi wa Nasa Raila Odinga mbali na kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa marufuku la NRM.