Jasusi wa shirika la kijasusi la Marekeni, Bill Oxley, ndiye binadamu pekee hadi sasa aliyekiri kuhusika moja kwa moja na kifo cha marehemu Bob Marley.
Akiwa katika kitanda cha hospitali ya Mercy huko Miami, Bill Oxley alitoa siri ya muda mrefu kuwa yeye ndiye aliyempa Bob Marley viatu aina ya raba ambavyo ndani yake viliwekwa sindano ndogo sana yenye ncha kali iliyokuwa na vimelea vya ugonjwa wa kansa.
Katika maelezo yake, Bill Oxley anasema alifanya hivyo ikiwa ni mpango wa Marekani kuwaua wanamapinduzi na wapigania uhuru duniani.
“Nilipewa jukumu hilo na kufanikiwa kuwa na urafiki na Bob Marley. Hii ilimfanya asiwe na shaka nilipompa zawadi hiyo ambayo ndoyo iliyoomua,” anasema Bill Oxley.
Katika maelezo yake Bill Oxley anaendelea kusema Bado anakumbuka na kuumia sana akijiwa na kumbukumbu ya namna Bob Marley alivyovaa raba hizo kwa furaha na kuhisi kama amechomwa na kitu. Hata hivyo hakuhisi chochote kwani alidhani ni raba zilikuwa zinambana kutokana na kuwa mpya.
Hivyo ndivyo marehemu Bob Marley alivyoambukizwa kansa iliyoanza kumdhoofisha taratibu hadi alipofariki tarehe 11 Mei 1981 akiwa anatibiwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Miami.
“Bob Marley alikuwa anafanikiwa sana katika kutumia muziki wake wa reggae kama silaha ya ukombozi. Muziki wake ulionekana kuwa ni hatari kuliko hata risasi na mabomu. Katika miaka ya 1976 Bob Marley alionekana kuwa ni hatari sana dhidi ya nguvu kubwa zilizofichika za dunia zilizodhamiria kuunda mfumo mpya wa namna ya kuiendesha dunia.
Kwa maana hii Bob Marley alistahili kufa ili mipango hii ipate kuendelea. Ingawa kifo chake kiliniuma sana lakini sijutii kwani nilikuwa natimiza wajibu wangu kama sehemu ya mpango mkubwa wa dunia.” alisema Bill Oxley