Mrembo wa Kenya, Ruth Kamande ambaye anatumikia kifungo jela kwa kosa la kumuua kwa kumchoma visu mara 22 mpenzi wake ameshika vichwa vya habari baada ya kushinda taji la Mrimbwende wa Jela (Miss Prison).

Mrembo huyo ambaye anatumikia kifungo chake katika Jela ya Lang’ata nchini humo, kabla ya kutunukiwa taji lake alieleza kujutia maamuzi yake ya hasira yaliyopelekea kumuua mpenzi wake baada ya kumkuta na ujumbe wa simu wa mapenzi kutoka kwa mwanamke mwingine.

Miss Lang'ata Prison,

Miss Lang’ata prison

Alihukumiwa kifungo hicho Septemba mwaka jana baada ya Mahakama kumkuta na hatia ya mauaji ya Farid Ahmed (aliyekuwa mpenzi wake), ameeleza kuwa anatamani muda ungerudi nyuma kwani asingechukua uamuzi huo.

“Wakati wote kuna njia bora zaidi ya kutatua migogoro kuliko kufikia hatua mbaya zaidi,” amesema mshindi huyo wa taji la mrembo wa jela ya Langata.

Mrembo huyo sasa amejiunga na program maalum ndani ya jela hiyo inayolenga katika kuwafunda wafungwa wa kike namna ya kuacha mienendo mibaya na kuwa watu bora zaidi.

Katibu Mkuu Wizara Ya Ujenzi Uchukuzi Na Mawasiliano Atoa Neno Kwa Vyuo
JWTZ Yalionya gazeti la Tanzania Daima kwa lilichoandika Septemba 1