Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mji wa Geita Modest Apolinary, kupisha uchunguzi  kufuatia ununuzi wa gari yenye dhamani ya shilingi millioni 400.

Waziri Jafo amesema  kuwa mara baada ya Bunge la 11 la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baraza la Madiwani kuvunjwa majukumu yote yalisimishwa kwa wakurugenzi na kupelekea baadhi ya  Halmashauri kutumia muanya huo kufanya ubadhilifu wa fedha za umma.

“Halmashauri ya Mji wa Geita, katika kipindi hicho ambacho baraza la madiwani halipo waliweza kununua gari lenye dhamani ya shilingi milioni 400, jambo hili halikubaliki kwa kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma”amesema Waziri Jafo

Waziri Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga, kuunda timu  ya uchunguzi  ambayo itachunguza kwa kina  matumizi ya fedha katika Halmashauri ya mji Geita.

Sambamba  na hilo amekiagiza kitengo cha ukaguzi Ofisi ya Rais-TAMISEMI  kufanya uchunguzi  na ufuatiliaji kwa Halmashauri  nyingine zenye kutiliwa shaka kama zilienda kinyume  cha taratibu ya matumizi ya fedha.

Bocco: Sina ugomvi na Kagere
Kocha Sven aridhishwa Simba SC