Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja katika Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, kuondolewa katika nafasi hiyo kutokana na majibu yasiyo stahiki wanayojibiwa Wananchi wanapopiga simu kwenye Shirika hilo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

Dkt. Biteko ametoa maagizo hayo wakati aliposimama katika Kijiji cha Msimbati wilayani Mtwara, Mkoa wa Mtwara ili kuzungumza na wananchi akiwa anatokea kukagua visima vya kuzalisha na mitambo ya kuchakata Gesi ya Mnazi Bay iliyopo katika Kata ya Msimbati wilayani humo.

Aidha, Dkt. Biteko pia ameagiza kuwa, miradi inapotekelezwa katika eneo lazima ibadilishe maisha ya wananchi, ikiwemo pia upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile Shule, Vituo vya Afya, Barabara na Maji.

“Changamoto zote mlizozieleza hapa nataka niwahakikishie kuwa zitashughulikiwa, nataka muone tofauti kuanzia sasa, kama Gesi Asilia inatoka hapa na inaendesha mitambo ya umeme kwa asilimia 65, haiwezekani wala haiingii akilini, watu hawa wakalia kituo cha Afya, Polisi, ubovu wa barabara, haiwezekani,” amesema.

DCEA, Wanahabari mshirikiane elimu Dawa za Kulevya - Dkt. Rioba
Msisubiri maafa kuchukua hatua wakati ni sasa - Rais Mwinyi