Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Njombe Oktoba 17,2023 imemhukumu, Juma Radsalaus Msemwa (27), kifungo cha miaka 180 Jela Mkulima kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu huko mtaa wa Kihesa kwa kuwafungia ndani na Kisha kutekeleza tukio hilo
Akisoma hukumu hiyo ya kesi CC No 53/2023 Hakimu mkazi wa Wilaya ya Njombe, Matrida Kayombo amesema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 30, 2023 huko Kihesa Wilaya ya Njombe kabla ya kufikishwa na Mahakamani na kupatikana na hatia.
Aidha, mshitakiwa alisomewa mashita yote sita na kupatikana na hatia kwa Makosa yote sita na amefungwa miaka 30 kwa kila kosa na kufanya jumla ya miaka 180 ambapo adhabu hiyo itakwenda kwa pamoja, ili iwe fundisho kwa wengine.