Mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Hapi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwateua katika nyadhofa mbalimbali kwa ajili ya kufanya naye kazi katika serikali yake ya awamu ya sita.

Amesema hayo leo leo Juni 15, 2021, Jijini Mwanza, katika mkutano wa Rais Samia na vijana unaofanyika jijini Mwanza.

Rc Hapi amemuahidi Rais Samia kuwa vijana wataendelea kumpa ushirikiano na kwamba yupo tayari kutumwa popote pale kwaajili ya kufanya kazi kwa kuwatumiakia Watanzania.

“Rais kwa niaba ya vijana wote ambao umekwishatuteua kwenye serikali yako, tungependa kukushukuru sana kwa imani yako kubwa kwa vijana, nchi yetu wakati inapata uhuru Baba wa Taifa alikuwa na miaka 39 na Mzee Kawawa alikuwa na miaka 35 leo unazungumza na kundi lililoshiriki katika nchi yetu kuhakikisha tunapata ukombozi,” amesema RC Hapi.

“Vijana sisi tutakuunga mkono, tutakutii, tutapokea maelekezo yako, tutafanya kazi usiku na mchana popote pale utakapotupeleka kuhakikisha dhamira yako kwa vijana na kwa Tanzania inaenda kutimia, unalo jeshi la vijana nyuma yako ambao wako tayari kukusaidia kuitekeleza Ilani ya CCM”.

Mapato yashuka mipakani
Mradi wa SGR Dar-Morogoro umekamilika