Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Afrians wamejipanga kuja na Ushangiliaji wa tofauti kwa kuwawezesha Mashabiki na Wanachama, watakaojitokeza Uwanjani Oktoba 08 kushuhudia mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa wa Sudan Al Hilal.
Young Africans inakwenda kwenye mchezo huo huku ikiwa inajiamini kutokana na kuwa na kikosi bora na imara, huku ikichagizwa na rekodi ya kuizaba Zalan FC ya Sudan Kusini jumla ya mabao 9-0, baada ya kucheza nyumbani na ugenini mwanzoni mwa mwezi huu.
Afisa Habari wa Klabu hiyo Kongwe Afrika Mashariki na Kati Ally Kamwe amesema, Uongozi wa Young Africans umesikia kilio cha Mashabiki na Wanachama wake kuhusu Bendera za klabu hiyo, ambazo walihitaji kwa ajili ua kuchagiza ushangiliaji wao wanapokua Uwanja wa Benjamin Mkapa katika michezo ya Kimataifa.
Amesema: “Tunakwenda kufanya tukio ambalo halijawahi kufanyika kwenye mpira wetu Tanzania. Wanaotaka kununua bendera mzigo upo tayari umeshafika, ni kuwahi tu kununua. Sio bendera tu tuna kila aina ya vikolombwezo vya ushangiliaji Kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Al Hilal”
“Siku hiyo tumeweka Viingilio rafiki kabisa, kwa hiyo hakuna sababu ya mtu kukosa. Lakini pia kama kumbukumbu zangu zipo sawa siku hiyo itakuwa ni sikukuu ya MAULID hivyo watu wajitokeze kwa wingi”
“Yanga ndio timu iliyojiandaa zaidi msimu huu kuiweka Tanzania mabegani na kuiwakilisha vyema kimataifa”
“Rai Yangu kwa wanahabari wote wanaoipamba sana Al Hilal ?? kama wamecheza fainali, wajue historia haichezi uwanjani”
“Nimesikitishwa sana leo, kumsikia mtu anasema timu ndogo zinaanzia nyumbani. Lakini namjibu kwanza lazima uwe na uwezo wa kufikiria kwa nini CAF wanapanga hivyo ndipo uongee”
“Kauli mbiu yetu ni ileile kwenye mchezo huu dhidi ya Al HilAL ‘IWE JUA IWE MVUA’.. Na kwa kuongezea IWE JUA IWE MVUA WATAPIGWA KAMA NGOMA”
“Tupo tayari sio tu kumuondoa Al Hilal ?? bali KUMSAMBARATISHA. Wale wanaosema tuna mlima mrefu wa kupanda, tunawaambia sisi ndio wapandaji”