Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Malindi vusiwani Zanzibar Ally Saleh (Alberto) ametangaza nia ya kuwania kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF).

Alberto ametangaza nia ya kuwania nafasi hiyo huku wadau wa soka wengine watano wakikamilisha zoezi la kuchukua fomu, sambamba na Rais Karia anaetetea nafasi yake.

Alberto amesema ana uzoefu wa kutosha katika soka la Tanzania, hivyo anajiamini kuwa kiongozi shupavu endapo atapewa ridhaa ya kuongoza kupitia wajumbe wa mkutano mkuu.

“Nitawania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF,
Uzoefu michezoni, Mjumbe Baraza la Michezo ZNZ, Katibu Shangani FC,”

“Nimewahi kuwa Wakala wa Wachezaji FIFA, Kiongozi vyama vya Chess, Mpira wa Meza, Mpira wa Kikapu, Mjumbe kamati mbali mbali za kitaifa, Mwandishi Habari, Mwanasheria”. Amesema Ally Saleh .

Mpaka sasa waliochukua fomu za kuwania kiti cha Urais wa TFF ni Wallace Karia, Deogratius Mutungi, Evans G. Mgeusa, Zahoro M. Hajji na Oscar Oscar.

Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika mapema mwezi Agosti jijini Tanga.

Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Botswana
Huu ndio mkakati wa kuchochea Uchumi shindani - Mwigulu