Almasi inayoaminika kuwa ya tatu kwa ukubwa kuwahi kupatikana yenye uzito wa karati 1,098, imewekwa kwenye maonesho nchini Botswana.

Jiwe hilo la thamani ambalo ni zito kidogo kuliko almasi ya pili ya ukubwa duniani ambayo pia ilipatikana Botswana mwaka 2015, lilioneshwa na Rais Mokgweetsi Masisi,  baada ya kampuni ya Almasi, Debswana, kuipata.

Debswana ni mshirika wa pamoja kati ya serikali na kampuni kubwa ya madini ya almasi duniani De Beers na hadi asilimia 80 ya kipato kinachotokana na mauzo hayo huelekezwa kwa hazina ya serikali kupitia pesa zinazolipwa kama faida, mrabaha na kodi.

Waziri wa madini nchini Botswana, Lefoko Moagi, amesema ugunduzi huo wa hivi karibuni umewasili wakati muafaka baada ya janga la virusi vya corona lililokumba Botswana kusababisha kupungua kwa mauzo ya almasi mwaka jana.

Juni 10,2021 Rais Masisi alikuja Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Rais Samia alisema Tanzania itapeleka timu ya watalamu kwenda Botswana kujifunza mikakati ya kuendeleza madini nchini, kwa ajili ya biashara duniani na kukuza uchumi wa nchi.

Botswana ndio mzalishaji mkubwa wa madini ya almasi Afrika.

TANZIA: Aliyekuwa Rais wa Zambia Keneth Kaunda afariki dunia, watu mashuhuri watuma salamu za pole
Mkataba kuandaa mitaala ya shule za ufundi kusainiwa