Manchester City imepanga kuingia vitani dhidi ya Real Madrid kuiwania saini ya beki wa pembeni wa Bayern Munich na Canada, Alphonso Davies dirisha lijalo la majira ya Baridi au Kiangazi.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Munich imekuwa ikipambana kumsainisha mkataba mpya ili kumzuia asiondoke.

Hata hivyo, Davies ameonyesha nia ya kutohitaji kusaini mkataba mpya na kusisitiza bado anataka kupambana ili kupata changamoto mpya sehemu nyingine.

Munich inafahamu ikiwa itashindwa kumshawishi asaini Davies, itatakiwa kumuuza dirisha lijalo la majira ya kiangazi msimu huu, kwani ikisubiri hadi Januari 2025 itakuwa kwenye presha ya kumpoteza bure, hivyo inaweza kumuuza kwa kiasi kidogo cha pesa.

Tangu kuanza kwa mwenye umri wa miaka 22, amecheza mechi 10 za michuano yote na kutoa asisti tatu.

Jamaa amekuwa akisifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupandisha mashambulizi kwa kasi na mashabiki wa soka Ujerumani wamebatiza jina la utani la pikipiki.

Wanawake, Wasichana Milioni 68 hatarini kukeketwa
Athari za Mvua: Maporomoko ya ardhi yauwa 23