Mwanamme mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel Ooko Alego wa nchini Kenya amefikishwa Mahakamani kutokana na kujihusisha na tukio la wizi nyumbani kwa jirani yake ambaye alimnyima nafasi ya kulala nyumbani kwake.
Katika rekodi za mahakama, mshtakiwa Daniel Ooko Alego, ambaye alikuwa pamoja na watu wengine wawili walinaswa kwenye kanda ya CCTV wakivunja na kuiba ndani ya nyumba ya Samuel Mutahi na wanasemekana waliiba vipakatalishi vitatu, simu ya mkononi na pesa taslimu.
Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Makadara M. Malingu, Mutahi aliiambia mahakama kuwa Alego alitenda kosa hilo mnamo Agosti 16, 2021, katika eneo la Clay City, mtaani Kasarani.
Mutahi alithibitisha kwamba aliondoka nyumbani kwake akiwa na mkewe asubuhi saa nne asubuhi siku hiyo.
“Nilirudi mwendo wa saa tatu usiku na kukuta mlango umevunjwa na vitu vimeibwa. Asubuhi iliyofuata, nilienda kumuarifu keyateka na kumuomba anipe picha za CCTV, “Hapo ndipo tulipomwona Alego na marafiki zake wawili; mwanamke na mwanamume wakifanya uhalifu katika nyumba yangu,” alisimulia Mutahi.
“Aliniomba nimruhusu kulala nyumbani kwangu kwa sababu alikuwa amepoteza kazi yake na hakuwa na pesa, lakini sikumruhusu,” mwathirika aliongeza.
Kesi hiyo itatajwa tena Februari 25,