Msanii Amber Lulu ametakiwa kuripoti kituo cha polisi cha Urafiki kilichopo Ubungo jijini Dar kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kusambaa kwa picha yake ya nusu utupu akiwa na msanii wa rap Yound D.

Picha hiyo ilisambaa jana kupitia mtandao wa instagram ambapo imeonesha Amber Lulu akiwa amesimama nusu utupu huku rapa Young D akiwa anaangalia maumbile yake.

Kupitia mtandao wa instagram Rapa Young ameomba radhi kwa mashabiki wake kuhusiana na  kuvujika kwa picha hiyo na kudai kuwa picha hiyo imevuja bila ridhaa yake.

Hivyo alitumia ukurasa wake na kuandika haya, ”Nasikitishwa kwa picha inayosambaa mitandaoni, imevuja bila ridhaa yangu ni picha iliyokua imepigwa behind the scene lengo haswa la photoshoot ni aina hii mpya ya mavazi ya aina ya ‘kiscottish’ kama sketi. Naomba radhi sana  kwa hili na kwa mashabiki wote! so sad.

kupitia hatua hiyo iliyochukuliwa na polisi inadhihirisha wazi kuwa sheria za mtandaoni zinafanya kazi, kwani kurusha picha ya utupu ni moja ya mambo yanayovunja sheria za mtandaoni.

 

Mahakama yamfutia shtaka aliyekuwa kiongozi UVCCM
Dkt. Mwakyembe: Michezo ni ajira ya kudumu