Mwanamuziki wa kizazi kipya Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu ameeleza kuwa wakati anaanza muziki kama mwanamuziki chipukizi watu wengi walikuwa hawamuamini katika kuimba na kumdharau.

Mwanamuziki huyo ambaye amepata mafanikio kupitia muziki wa bongo fleva amesema kuwa muziki umebadilisha maisha yake kwa asilimia kubwa amesema kwasasa anapokea simu nyingi kutoka kwa watu kwaajili ya kazi.

”Vitu vingi sana vimebadilika kutokana na muziki ‘lifestyle’ muonekanao kuvimba, na wanaonichukia, pesa ndio kila kitu, wakati naanza muziki watu wengi walinichukulia poa sana walikuwa wanaona siwezi muziki nitaacha tuu”’alisema amber lulu

Msanii huyo ameendelea kusema kuwa watu ambao walikuwa wanamsema sasa hivi wamegeuka na kumkubali, kwa kumuomba msaada  na kutambua nini anafanya  na wengineo wamekuwa mashabiki zake na chawa wake ameleza msanii huyo.

 

 

Nkana yatoa adhabu kali kwa mashabiki waliorusha mawe
Video: Rugemarila ayakataa mabilioni ya Tibaijuka, Vituko vya viongozi wateule