Maafisa wa polisi nchini Uganda wamemkamata dereva mmoja ambaye alipigwa picha akishusha mananasi kutoka kwenye gari ya wagonjwa ya Hospitali ya Kebisoni Center IV wilayani Rukungiri.

Kulingana na msemaji wa polisi wa eneo la Kigezi, Elly Maate, dereva huyo kwa jina Matayo Barekye ni mkazi kutoka mjini Kebisoni, wilaya ya Rukungiri.

Daily Monitor inaripoti kuwa Barekye alinaswa kwenye picha mnamo Januari 27, 2022, katika soko la Nyamunuka akishusha mananasi kutoka kwa ambulensi yenye usajili wa nambari ya UG 3797M.

Barekye anadaiwa kusafirisha mananasi baada ya kumfikisha nyumbani mgonjwa ambaye aliyefanyiwa upasuaji na akiwa safarini kurejea, aliamua kubeba mzigo wa mananasi na wakati alipokuwa akiushusha alipigwa picha na kuzua ghadhabu mtandaoni.

“Polisi walimkamata mshukiwa huyo baada ya picha za kupakuliwa kwa mananasi kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi yametajwa dhidi yake,” alisema Maate.

Msemaji wa polisi pia aliongezea kuwa dereva huyo mwenye umri wa miaka 50, atashtakiwa na matumizi mabaya ya ofisi na aliwataka watumishi wa umma kuzingatia maadili yao siku zote ili kuepuka visa hivyo vinavyosababisha matumizi mabaya ya ofisi.

Tukio hilo ni sawia na moja nchini Kenya ambapo ambulensi ilitumika kuwasafirisha vijana walevi wakati wa kafyu. Katika video hiyo iliyosambaa sana, kundi la vijana walevi linaonekana likipiga kelele likiwa ndani ya ambulensi hivyo. Kufuatia kisa hicho, EMS Kenya ambayo inamiliki ambulensi hiyo ilitoa taarifa siku ya Jumamosi, Aprili 18, ikidai kwamba hatua za kinidamu zimechukuliwa dhidi ya wafanyakazi wake ambao walihusishwa kwenye video hiyo.

Ugiriki, dereva wa gari la wagonjwa alinaswa akisafirisha bangi yenye thamani ya dola milioni 6.3 kwenye mpaka wa Ugiriki na Albania akiwa na mifuko 13 ya duffle iliyokuwa na pakiti 129 za bangi.

Harakati za uchaguzi Kenya:Ruto amtaka Kenyatta kukumbuka fadhila
Zuchu, Mbosso kundi moja Burna Boy na Davido