Bondia kutoka nchini England, Amir Khan huenda akapambana na Manny Pacquiao, baada ya kushindwa kutimiza ndoto zake za kupanda ulingoni na bingwa wa dunia Floyd Mayweather aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa juma lililopita.

Mzungumzo kuhusu mpambano wa Khan dhidi ya Pacquiao yanaendelea kwa sasa kwa kushirikisha viongozi wa pande zote mbili.

Tayari tetesi zimeenza kujitokeza katika mitandao ya kijamii zikieleza kwamba huenda wawili hao wakakutana ulingoni mwezi Novemba mwaka huu huku wengine wakidai pambano hilo litakua la mwisho kwa Pacquiao ambaye tayari ameshaeleza itakapofika mwaka 2016 ataachana na mchezo wa masumbwi.

Khan amekua kimya tangu alipomkandamiza mpinzani wake kutoka nchini Marekani Chris Algieri mwezi may mwaka 2015, na alionyesha dhamira ya kutaka kupanda ulingoni dhidi ya Floyd Mayweather, lakini aliweka masharti ya kutaka kupewa nafasi ya kutimiza ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo Khan, bado ameonyesha dhamira ya kumuhitaji Mayweather, kwa kusema anaamini atabadili msimamo wake wa kustaafu mchezo wa ndondi ili arejee ulingoni na kukamilisha pambano la 50 ambalo amependekeza limkutanishe nae.

Kwa upande wa Manny Pacquiao, hajarejea tena ulingoni tangu alipopoteza kwa point dhidi ya Floyd Mayweather katika pambano lililounguruma May 02 mwaka huu.

Mayweather alitangaza kuachana na ndondi mara baada ya mpambano wake dhidi ya Andre Berto aliyemshinda kwa point.

Historia inaonyesha kwamba Mayweather anakua bondia aliyetangaza kujiweka pembeni huku akiwa ameshinda michezo 49 pasi na kupoteza hata mmoja.

Tanzania Yaambulia Patupu All African Games
Joh Makini Aeleza Sababu Za Kutojihusisha Na Kampeni Za Siasa