Bondia Muingereza, Amir Khan amefungiwa miaka miwili baada ya kubainika kutumia dawa zinazokatazwa michezoni katika pambano lake dhidi ya Kell Brook, lililopigwa mwezi Februari 2022.

Bingwa huyo wa zamani wa Dunia wa uzito mwepesi, alikutwa na vimelea vya matumizi ya dawa aina ya ostarine.

Khan, ambaye alistaafu ngumi Mei mwaka jana, alikiri kuvunja kanuni za matumizi ya dawa zinazokatazwa michezoni lakini alisema haikuwa dhamira yake.

Arsenal, Man City kazi bado mbichi England

Oktoba mwaka jana, Muingereza CJ Ujah alifungiwa kwa miezi 22 baada ya vipimo kuonesha ametumia dawa zinazokatazwa michezoni ikiwemo ostarine kwenye michezo ya Olimpiki, Tokyo. Vifungo katika michezo yote ilitakiwa kuanza Aprili 6, 2022 mpaka Aprili 5, 2024.

Khan, ambaye alishinda medali ya fedha kwenye michezo ya Olimpiki mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 17, alipigwa na Brook kwa KO katika raundi ya sita katika pambano hilo ambalo alithibitisha lilikuwa la mwisho kwake.

Alistaafu mchezo huo miezi mitatu baadae, akimaliza kwa kushinda mapambano 34, kupoteza sita tangu aliporudi kwenye ngumi za kulipwa mwaka 2005.

Nje ya ulingo ameendelea kutunza umaarufu wake akifanya kipindi cha runinga Australia kikiitwa I’m a Celebrity…. Get Me Out of Here! Na pia ana kipindi kwenye BBC kikiitwa ‘Meet the Khans: Big in Bolton’.

Pia anatarajia kuonekana kwenye I’m a Celebrity katika kituo cha runinga cha Afrika Kusini baadae mwezi huu.

Watu 805 wapewa elimu ugonjwa wa Marburg Magereza
Malalamiko ya Wananchi yamfikisha Waziri Jafo Bahi