Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2015/16, Amissi Jocelyn Tambwe ameamua kuongelea kuhusu watu wanaomshindanisha na mshambuliaji mpya wa Simba , Laudit Mavugo  huku akisisitiza kuwa ubishi huo utajibiwa mara baada ya Ligi Kuu msimu mpya kuanza.

Hivi karibuni umeibuka mjadala miongoni mwa wadau wa soka kuhusiana na wachezaji hao hususani mashabiki wa Young Africans na Simba ambapo kila upande unadai mchezaji wao ni mkali zaidi kwenye upachikaji mabao.

Mjadala huo umeibuka baada ya Mavugo ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Vital’O ya Burundi kujiunga na Simba katika kipindui sha usajili ambacho kilifungwa rasmi mwishoni mwa juma lililopita.

Rekodi za wachezaji hao ndio zinachochea kuwapo kwa mjadala huo ambapo Tambwe alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita baada ya kupachika mabao 21.

Tambwe amesema hawezi kumzungumzia Mavugo na badala yake ligi ndiyo itakayoamua nani mkali kati yao kwenye kucheka na nyavu.

laudit-mavugoLaudit Mavugo

“Wengi wananiuliza mimi na Mavugo nani zaidi kwenye ufungaji, kiukweli kila mmoja atavutia kwake katika hili, lakini ligi ndiyo itakayoamua.

“Binafsi nina mipango mingi msimu ujao ikiwemo kuisaidia timu yangu kutetea taji lake, pia nahitaji kutwaa tuzo nyingine ya ufungaji bora, hayo naweza kuyatimiza kwa uwezo wa Mungu,” alisema mshambuliaji huyo.

Mzee Akilimali Amesimamishwa Kwa Muda Usiojulikana
Rais wa Zambia atangazwa kushinda uchaguzi, wapinzani wang’aka