Mwalimu Joseph Msafiri, wa shule ya msingi Namagubu mkoani Mwanza, anashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumkata mapanga mpenzi wake, Neema kabulu (19) mkazi wa Ukerewe na kumjeruhi vibaya walipokuwa njiani kuelekea kumtambulisha ukweni.

Tukio hilo limetokea juzi usiku eneo la old Shinyanga mjini, wakati mwalimu huyo akiwa amelala na mpenzi wake kwenye nyumba ya wageni ili kesho yake kwenda kumtambulisha ukweni Iselamagazi shinyanga vijjini, ndipo ugomvi baina yao ukatokea.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Richard Abwao, amesema kuwa mwalimu huyo alimkata mapanga mpenzi wake maeneo ya usoni, tumboni na mkono wa kulia, hivyo alikimbizwa kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya rufani ya mkoa huo, na haliyake bado ni mbaya.

Kamanda Abwao amesema Mwalimu Msafiri alikwenda na mpenzi wake kwaajili ya kumtambulisha kwa wazazi wake lakini ukatokea ugomvi kati yao ambao chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa kimapenzi, kutokana na mwalimu huyo kumtuhumu mpenzi wake kuwa siyo mwaminifu kwenye mahusiano yao.

” kwenye eneo la tukio yalipotokea mapigano hayo, tulikuta panga lililokuwa limetumka kumshambulia mwanamke huyo pamoja na nguo zenye damu” amesema kamanda Abwao.

Aidha amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia mwalimu huyo na kwamba taratibu nyingine zikishakamilika atafikishwa mahakamani.

Sancho kuikabili Kosovo
Mugabe kuagwa Jumamosi, mazishi yaandaliwa