Uongozi wa Klabu ya Mbeya City umesitisha rasmi mkataba na kocha Amri Said baada ya makubaliano ya pande zote mbili kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu 2020/21.

Timu hiyo inayokamata mkia kwenye msimamo wa ligi, itakuwa chini ya kocha wake msaidizi Mathias Wandiba wakati taratibu za kupata kocha mpya zikiendelea. Hadi sasa ikiwa imecheza mechi saba, imetoka sare mechi mbili , imepoteza tano na haijashinda mchezo wowote, ikiwa imefunga goli moja pekee.

Simba SC: Tupo tayari kuwavaa Tanzania Prisons
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 21, 2020