Mwanaume mmoja raia wa Marekani Grant Amanto (29), mwenye hisia kali za mapenzi dhidi ya mwanamke aliyemuona mtandaoni aliyefahamika kwa jina moja la Sylivia, amewauwa wazazi wake pamoja na kaka yake, kwa kile kilichodaiwa kuingilia kati mapenzi yake na mpenzi wake aliyemuona mtandaoni.

Wawili hao hawakuwahi kukutana bali walikuwa wakiwasiliana kupitia mtandao wa Twitter na Skype, ambapo kijana huyo alimlaghai mrembo huyo kwa kujifanya anauwezo mkubwa wa kifedha huku kiuhalisia alikuwa akiiishi katika nyumba ndogo ya wazazi wake, mjini Chuluota, Florida .

kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Polisi mjini humo, familia ya Grant ilibaini kijana wao aliiba pesa za mkopo uliochukuliwa na wazazi wake kiasi cha Dola za Kimarekani 150000, na mara baada ya wazazi kugundua hilo walimlazimisha kijana wao amwambie ukweli Sylivia juu ya hali yake ya kipato, ambapo mwenyewe alidai jambo hilo lilikuwa ni udhalilishaji kwake.

Siku ya tukio Grant alianza kwa kumuua Mama yake Marget (61), kisha Baba yake Chad (59) na hatimaye alimaliza kwa kufanya mauwaji ya kaka yake Cody (30).

Wahujumu uchumi 467 watubu, bilioni 107 kurudishwa
Metacha Mnata akiri mambo magumu Yanga