Mahakama nchini Hispania imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela Alberto Sanchez Gomez (28), baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mama yake na kumla nyama huku akikutwa na mabaki ya mwili wake.
Vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa Gomez alikuwa anajulikana na maofisa wa Polisi kutokana na ghasia dhidi ya mama yake na kwamba alikuwa amekiuka agizo la kumkamata.
Maofisa wa Polisi waliwasili katika nyumba ya mama yake huyo Februari, 2019 baada ya rafiki wa jamaa huyo kuwasilisha malalamiko juu ya mauaji ya Maria Soledad Gomez ambaye alikuwa na umri wa miaka 60.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, mahakama ilielezewa kwamba Sanchez, wakati huo akiwa na umri wa miaka 26 alimyonga mama’ke wakati wa mzozo.
Atatumikia kifungo cha miaka 15 kwa mauaji na miezi mingine mitano kwa uharibifu wa mabaki ya mfu. Pia ametakiwa kulipa faini ya Dola za Kimarekani 73,000 kama fidia.
Gomez alikamatwa mwaka 2019 baada ya maofisa wa Polisi kupata mabaki ya mwili katika nyumba ya mama’ke huku mengine yakiwa katika plastiki.
Baadaye aliukatakata mwili wa mamake na kuula huku vipande vingine akiwalisha mbwa.