Jeshi la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Ramadhani Habibu, mkazi wa kijiji cha Vilabwa, wilaya ya Kisarawe, kwa kudaiwa kumchoma kisu mwenzake chanzo kikiwa ubishani wa makalio ya mwanamke aliyepita njia .

Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa polisi mkoani hapo, Jonathan Shanna ambaye ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa kosa la mauaji.

Ramadhani anadaiwa kumuua, Emmanuel Nassor (26) kwa kumchoma na kisu kifuani baada ya kutokea ubishi kati yao kuhusu ukubwa wa umbo lake la nyuma ‘tako’ la msichana aliyewapita wakipiga soga kijiweni.

“Kuna mdada alipita sasa marehemu na mtuhumiwa walikuwa na wenzao kijiweni wakaanza kuzozana kuwa yule mdada ana ‘Chura’, wengine wakasema la kawaida” amesema Kamanda Shanna

Kamanda Shanna, amesema ubishi ulikuwa mkubwa ndipo Ramadhani kwa hasira, akakimbia nyumbani kuchukua kisu alichokitumia kumchoma mwenzake hadi kumuua.

Amesema mtuhumiwa alikimbia ambapo siku ya Septemba 27 majira ya saa 2 asubuhi alikamatwa.

Kamanda huyo, aliwaasa vijana kuacha tabia ya kupoteza muda vijiweni badala ya kujishughulisha kimaendeleo.

 

Video: INAUMA SANA! Binti mwenye ugonjwa wa ajabu asimulia mazito, apaza sauti kuokoa maisha yake

JPM atoa milioni 260 kujenga nyumba za Jeshi la Polisi zilizoungua Arusha
Issa Abdi Makamba atibiwa Dar