Mtu mmoja, Jackie Rahm Little  (36), anashikiliwa na Polisi wa Minneapolis nchini Marekani, akishukiwa kuwasha moto ulioharibu msikiti jijini humo katika jaribio la kuanzisha vitisho  kwa jamii ya Kiislamu.

Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Brian O’Hara amesema Little alitenda kosa hilo Aprili 24 na 24, 2023 na alikamatwa hapo jana Jumapili Aprili 30, 2023 na kusema atashitakiwa kwa kuchoma moto jengo takatifu, ambako familia na watoto hukusanyika.

Viongozi walio katika baraza la Mahusiano ya Kislamu na Marekani wa Minnesota walipongeza kukamatwa kwa mtu huyo baada ya tukio la moto ambalo wanadai halikuwatia hofu.

Picha: Rais Samia katika sherehe za Mei Mosi
Ahmed Ally: Tunaamini katika mafanikio