Chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) kimekutana kwa ajili ya kufanya mkutano mkuu wa kumchagua kiongozi mpya atakayerithi nafasi ya Jacob Zuma aliyekiongoza chama hicho kwa muda mrefu.

Baadhi ya vyanzo vya habari nchini humo vimesema kuwa mwelekeo wa chama hicho tawala umekuwa ukiyumba na kupoteza umaarufu kutokana na kashfa za rushwa na mipasuko ya kisiasa ndani ya chama.

Aidha, taarifa iliyotolewa na ANC imesema kuwa wajumbe wanatarajiwa pia kuwachagua viongozi sita wa ngazi ya juu kuanzia rais wa chama hadi naibu katibu mkuu wa chama.

Hata hivyo, ushindani unatarajiwa kuwa mkali kati ya aliyekuwa mke wa zamani za Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma aliyewahi kuwa waziri na pia kutumikia nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika na makamu wa sasa Cyril Ramaphosa.

 

 

Mnangangwa: Huu si wakati wa kutambiana na kusifiana
Msigwa: Hata mkinitisha sihami chama