Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini leo kimeweka historia kwa kumchagua Cyril Ramaphosa kuwa mwenyekiti wake.
Ramaphosa alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika leo akipata ushindi mwembamba dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu, Nkosazana Dlamini-Zuma aliyekuwa mke wa Rais Jacob Zuma.
Msimamizi wa uchaguzi huo alimtaja Ramaphosa kuwa mshindi akipata asilimia 51.8 ya kura zote halali zilizohesababiwa, akimzidi mpinzani wake kwa takribani kura 200.
Ushindi huu unampa nafasi Ramaphosa kuwa mrithi wa kiti cha urais endapo atashinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.
Uchaguzi huo umekata mzizi wa fitna ndani ya chama hicho kufuatia mgogoro mkubwa wa madaraka uliopelekea pande mbili hasimu za Dlamini-Zuma na Ramaphosa kufikishana mahakamani.