Kocha Carlo Ancelotti alimsifu Jude Bellingham ana kiwango bora baada ya kiungo huyo wa kati wa England kufunga na kumfanya kuwa mchezaji bora kwenye mechi yake ya kwanza ya ushindani akiwa na Real Madrid katika ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Athletic Club hapo juzi.
Rodrygo aliifungia Madrid bao la kuongoza dakika ya 28 mjini Bilbao kabla ya Bellingham kuongeza bao la pili dakika nane baadaye.
Mabao hayo yaliipa Madrid pointi zote tatu katika mchezo wao wa ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Hispania, LaLiga, huku mlinzi Éder Militão akichechemea kwa kilio kipindi cha pili kutokanà na jeraha la goti.
“Bellingham ni bora,” alisema Ancelotti katika mkutano wake na waandi- shí wa habari baada ya mechi.
“Ni mchezaji mzuri na mwenye haiba kubwa, ni mchezaji mwenye ubora. Ni usajili muhimu sana. Ana tabia thabiti, anahisi kama amekuwa hapa kwa muda mrefu.”
Madrid ililipa Euro milioni 103 za awali, na uwezekano mwingine wa Euro milioni 30 katika vigezo kumsajili Bellingham mwenye umri wa miaka 20 kutoka Borussia Dortmund msimu huu wa joto, akiwa nyongeza yao kwenye kikosi pamoja na Arda Güler, Joselu, Fran García na Brahim Díaz.
“Siku zote nimefundishwa kuwa ukijaribu kugonga shabaha basi unajipa nafasi,” Bellingham aliiambia Real Madrid TV alipoulizwa kuhusu bao lake la kwanza.
“Sikuwa, na mawasiliano mazuri, nilipata bahati kidogo, lakini nilifikia lengo.