Mlinda Lango Andre Onana Rasmi ametangaza kustaafu kuitumiki Timu ya Taifa ya Cameroon ‘Indomitable Lions’, baada ya kundolewa kweye Kambi ya timu hiyo, wakati wa Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar.
Onana mwenye umri wa miaka 26 alicheza mchezo mmoja dhidi ya Uswiz, na baadae alitofautiana kauli na Kocha Mkuu Rigobert Song na kuamriwa kuondoka kambini.
Hata hivyo hadi sasa Uongozi wa Shirikisho la soka nchini Cameroon ‘FECAFOOT’ na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa hawajafafanua tatizo lililopelekea Onana kuondolewa kambini.
Mapema leo Ijumaa (Desemba 23), Milinda Lango huyo wa klabu ya Inter Milan ya Italia, aliandika katika Ukurasa wake wa Instagram akithibitisha kustaafu kuitumikia Timu ya taifa ya Cameroon ‘Indomitable Lions’.
Onana ameandika: “Baada ya masaa mengi ya mafunzo, safari zisizo na mwisho na uvumilivu mwingi, naweza kusema kwa moyo kuwa nimetimiza ndoto yangu kubwa.”
“Hadithi hata iwe nzuri vipi, lazima iwe na mwisho.”
Hadi anatangza kustaafu, Onana ameshaitumikia Timu ya Taifa ya Camerron ‘Indomitable Lions’ katika michezo 34, huku akiitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016.