Mabingwa wa kihistoria barani Ulaya Real Madrid, wameanza vibaya harakati za kuwania taji la bara hilo msimu huu wa 2019/20, kwa kuchapwa mabao matatu kwa sifuri na Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa.

Real Madrid wanaotamba barani humo kwa kutwaaa taji la ligi ya mabingwa mara 13, walipokea kichapo hicho wakiwa ugenini jijini Paris usiku wa kuamkia leo, huku mchezaji wao wa zamani Angel di Maria, akiwashangaza kwa kufunga mabao mawili, dakika ya 14 na 33.

Bao lingine la PSG lilifungwa na Thomas Meunier, dakika ya 90, huku Gareth Bale akikosa mkwaju wa penati kipindi cha kwanza, ambao huenda ungewafuta machoji Real Madrid.

Di Maria alieitumikia Real Madrid kwa misimu mitano kabla ya kujiunga na Manchester United na baadae kutimkia jijini Paris, alikuwa nyota wa mchezo huo wa Kundi A, ambao ulifuatiliwa na mashabiki wengi ulimwenguni kote.

Licha ya PSG kutokuwa na nyota wake watatu Neymar, Edinson Cavani na Kylin Mbappe, lakini timu hiyo ilicheza kwa nidhamu dakika zote 90.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo:

Kundi A

Club Brugge 0 – 0 Galatasaray

Kundi B

Olympiacos 2 – 2 Tottenham Hotspur

Bayern Munich 3 – 0 FK Crvena Zvezda

Kundi C

Dinamo Zagreb 4 – 0 Atalanta

Shakhtar Donetsk 0 – 3 Manchester City

Kundi D

Atletico Madrid 2 – 2 Juventus

Bayer Leverkusen 1 – 2 Lokomotiv Moscow

Kimbunga cha Europa League kutimka leo
Video: Teknolojia itakayofichua tabia ya mlinzi wako, kumneemesha - PSGP