Familia ya waigizaji wa ‘Mr. &Mrs Smith’, Angelina Jolie na Brad Pitt wanatarajia kuongeza ukubwa wa familia yao kwa kuasili mtoto kutoka nchini Syria.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichoongea na Radar Online, wanandoa hao wenye watoto sita wanamalizia taratibu za kumuasili mtoto mmoja yatima kutoka kwenye familia ya watoto watatu yatima ambao wazazi wao walichukuliwa na wanajeshi wa Syria.

Inaelezwa kuwa Jolie ambaye anafanya kazi kama Balozi wa Umoja wa Mataifa wa ngazi za juu anaehusika na wakimbizi, alitembelea vituo sita vya wakimbizi nchini Syria ambapo alikutana na familia ya watoto hao watatu ambao baba yao alichukuliwa na wanajeshi wa Syria, mama yao aliuawa na nyumba yao iliharibiwa kwa bomu.

Inaelezwa kuwa kwa huruma, alitaka kuwaasili wote wa tatu lakini mumewe aliweka pingamizi na kumueleza kuwa itakuwa vigumu kwa watoto hao kuendana na mabadiliko ya haraka kiasi hicho ya kifamilia.

Arsene Wenger Aachana Na Mkewe
Gabriel Paulista Yupo Huru Kucheza