Wanandoa mastaa wa filamu, Brad Pitt na Angelina Jolie,wametajwa na gazeti na mtandao wa Observer’s LA Power 25 kuwa watu maarufu wenye nguvu zaidi Holywood.

Katika orodha ya mastaa 25 wenye nguvu zaidi waliotajwa na mtandao huo ikiongozwa na waigizaji hao wa filamu ya Mr &Mrs Smith, imewamtaja pia mtangazaji wa talk show maarufu, Ellen DeGeneres pamoja na Steven Spielberg.

Observer’s LA Power 25, wameelezea kuwa maana ya kuwa na nguvu katika orodha hiyo ni kuwa watu wanaoweza kuifanya jamii ya dunia hii kuongelea kitu fulani ama kutweet kwa wingi zaidi kuhusu kile walichokifanya.

“Hawa ni watu wanaotutengeneza kipi tuangalie kwenye TV na kipi tusikilize, kipi tunatweet pamoja na mavazi tunayovaa. Tunaenda wapi na tutazungumzia nini huko tuendapo.” Wameeleza.

Nicki Minaj Ampa Sharti Meek Mill Ili Amzalie Mtoto
Mchumba wa Luteni Karama Amshukia Inspector Haroun