Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema kuwa Angola imewafukuza wakimbizi kutoka nchini Congo DR, ambao walikimbia machafuko nchini mwao.

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Babar Baloch amesema kuwa wakimbizi hao wanalazimishwa kuvuka mpaka na kurudi nchini mwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,

Amesema kuwa takribani watu 200,000 wamewasili nchini mwao huku wakiwa hawana furaha na wengine kuonekana kukata tamaa.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari huko Geneva nchini Uswisi, msemaji huyo amesema kuwa shirika hilo lina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa migogoro katika mkoa wa Kasai ambako hali tayari ni tete.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kumekuwa na taarifa za mapigano na vurugu kati ya wahamiaji na mawakala wa utekelezaji wa zoezi hilo la kuwafukuza raia hao wa Kongo.

 

Serikali kufunga Kamera majiji yote nchini
Kanye West atoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima